Pages

Thursday, July 14, 2016

NYOTA WA JOYOUS CELEBRATION AZIDI KUPATA MAFANIKIO



Mwimbaji nyota kwasasa wa Joyous Celebration kijana Sibusiso Noah Mthembu ambaye amepata mafanikio ya kukubalika katika medani ya muziki wa injili nchini humo kwakupata mialiko mingi sambamba na kuwa mmoja wa waimbaji nyota ambao nyimbo zao zimetokea kuwagusa sana wapenzi wa muziki wa injili. Hivi karibuni anatarajia kuanza kuonekana akitangaza kipindi maarufu cha runinga Dumisa kiitwacho Imvuselelo kinachopatikana DSTV chanel ya 340 ambapo mwimbaji huyo amesema atatoa taarifa zaidi kuhusiana na kipindi hiki wakati muafaka ukifika

Kutangaza kwake kuwa mtangazaji kulipokelewa kwa shangwe na mashabiki wake pamoja na waimbaji na wapigaji wa muziki wa injili Afrika ya kusini ambao kwa pamoja wamempongeza mwimbaji huyo ambaye licha ya kwamba ni mwimbaji lakini pia ana elimu nzuri ya chuo kikuu ambako anashiriki kama assistant lecturer katika chuo kikuu cha Witwatersrand kilichopo jijini Johannesburg nchini humo.

Kama haitoshi mwimbaji huyo ambaye anatarajia kuungana na waimbaji na wapigaji wa zamani wa
Sibusiso alipokabidhiwa gari hilo na Lexus
Joyous Celebration kwa huduma katika majiji ya Leicester na London nchini Uingereza wiki ijayo, kuna taarifa kwamba kampuni inayotengeneza magari aina ya Lexus nchini Afrika ya kusini ilimzawadia gari ya kisasa mwimbaji huyo ambaye awali kabla ya kukabidhiwa gari hilo alikuwa anaweka picha mbalimbali za aina ya magari ya Lexus na kuyasifia kwa jinsi yanavyoonekana huku akimuomba Mungu ndoto yake kutimia ili kumiliki moja ya magari hayo ambapo Mungu alisikia maombi hayo na kukabidhiwa gari hilo ambalo amekuwa akilitumia siku za karibuni huku akiendelea kuyatangaza magari ya kampuni hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook. 




Sibusiso akiwa na gari lake
Mpaka sasa Sibusiso amesharekodi nyimbo nne na Joyous ambapo nyimbo zote zimetokea kukubalika na kupokelewa vyema na mashabiki wa Joyous na wapenzi wa muziki wa injili kwa ujumla lakini pia akisifika kwa uchezaji na uchangamfu popote pale kundi hilo linapotoa huduma.


Wimbo wa kwanza kurekodi na Joyous Celebration 17 Unkulunkulu


Credit:gospelkitaa

No comments:

Post a Comment